Office Address

123/A, Miranda City Likaoli Prikano, Dope

Phone Number

+0989 7876 9865 9

+(090) 8765 86543 85

Email Address

info@example.com

example.mail@hum.com

Michezo imekuwa nyenzo kubwa katika kuufikia mpango wa maendeleo endelevu wa mwaka 2030. Mkoani Kagera shirika la Jambo For Development lililojulikana kama Jambo Bukoba hapo awali linatumia michezo maalumu iliyotengenezwa kwa lengo la kufikisha elimu kwa watoto juu ya masuala ya Usawa wa Kijinsia, Afya Bora na Virusi vya Ukimwi. Walimu wa michezo ushiriki mafunzo haya ya michezo na kisha kupeleka utaalamu huo kwa wanafunzi shuleni na hatimaye kila mwisho wa mwaka  mashindano ufanyika yajulikanayo kama “Bonanza”.

Hadi hivi sasa ni jumla ya shule za msingi 48 hadi mwaka 2019 zimeshiriki Bonanza katika ngazi ya Wilaya ikiwa ni katika halmashauri zote 8 za mkoani Kagera. Kila halmashauri amepatikana mshindi mmoja ambaye ataiwakilisha halmashauri yake katika Bonanza la Mkoa lifayikalo  mwanzoni mwa mwaka, Ushindi wa shule husika katika Wilaya ni hatua ya kupata donge nono la kufanya mradi usiopungua shilingi milioni 44 (44,000,000Tsh) ambazo shule husika kupitia kamati yake pamoja na jamii husika huchagua aina ya mradi utakaofanyika kutokana na uhitaji wa shule husika na katika mradi husika jamii huchangia asilimia 10% ya mradi mzima, Serikali asilimia 30% na mfadhili 60% ili kuleta hali ya umiliki na kuhakikisha mradi ni endelevu.

Katika Mabonanza yaliyofanyika katika halmashauri zote nane. Shule washindi upata nafasi ya kushiriki katika bonanza la mkoa abalo ufaynika katika juma la mwisho la mwezi januari. “Tizama Wanafunzi hawa wanavyokuwa mashujaa katika jamii kwa kuleta miradi ya maendeleo katika Shule zao, wanaweka alama isiyofutika kamwe na hii ni ishara nzuri ya kuwa watoto wa kike na wakiume wanashiriki kuleta maendeleo yao wenyewe” Alisema Lameck Kiula Afisa Mawasiliano wa Shirika la Jambo For Development.