Shadia Mbaraka – Mjasiriamali
Tangu kuwepo kwa Ugonjwa wa korona athari kwa wafanyabiashra wakubwa na wadogo zinatofautiana ambapo kwa makaampuni makubwa kumekuwa na tatizo la kupungua kwa wateja na hivyo kupelekea makampuni hayo kupunguza wafanyakazi. Hali ilivyo kwa wafanyabiashara wadogowadogo kama machinga, bodaboda na mama lishe wao wanakutana na changamoto ya upungufu mkubwa wa wateja kulinganisha na hali ilivyokuwa hapo awali.
“Tumeathiriwa mno katika biashara zetu, kazi yangu hii ya kuuza chai hapa mtaani kwetu inazidi kuwa na chanagamoto wateja hawaji kama zamani wanahofu ya kuambukizwa ugonjwa wa korona licha ya kuwa nimefunga kibuyu chirizi na ninahimiza wateja wachache wanaokuja waweze kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kabla ya kupata huduma ila bado idadi ya wateja wa sasa sio kama ya zamani, ambapo sio chini ya wateja ishirini waliweza kufika kupata kifungua kinywa ila hivi sasa sio zaidi ya wateja nane hadi kumi pekee”. Anaeleza Shadia Mbaraka Mama lishe katika kijiji cha Lukole.
Shadia akiwa katika jiko lake akiandaa vitafunwa
Licha ya binti huyu mjasiliamali kutokata tamaa na kuendelea kufanya biashara hii ya mama lishe bado anaiona fursa na kuamini kuwa kama maelekezo na taarifa sahihi zitatolewa na kuwafikia watu kwa muda sahihi basi hata tofu iliyo wajaa watu itawaondoka na maisha yatarejea kama awali. “Najua ni hofu na hii ni kwasababu watu wengi huku kijijini hawana taarifa au elimu ya kutosha kuhusu huu ugonjwa huu kwa sababu watu bado wanasalimiana kwa kushikana mikono pamoja na kutofuata taratibu za kuacha hatua kati ya mtu mmoja na mwingine”
Wateja wakubwa wa Shadia ni madereva wa pikipiki ambao huegesha pikipiki zao katika eneo hilo. Anaeleza” Korona imechangia kuzorota kwa mzunguko wa pesa ni ngumu sana kupata shilingi elfu kumi kwa sasa wateja hawaendi maeneo ya mbali kama mjini na sokoni au hata wakienda wanatumia baiskeli na wengine wanatembea sielewi hii hali itaisha lini. Hata katika familia yangu watoto wamefunga shule na haijulikani bado itafunguliwa lini maana hata usomaji wao umekuwa wa tabu sana”
Kutokana na uwepo wa taarifa iiyosambaa kutoka mkoa wa Ruvuma juu ya ongezeko la mimba za utotoni kwa wanafunzi kwa miezi miwili mfululizo ilichochea mno hisia za kijana mmoja ambaye ni dereva pikipiki na kusema “Watoto sio wa mtu mmoja tu, na katika kipindi hiki ambacho watoto wako likizo ni muhimu sana kila mmoja kuwalinda na kuhakikisha wako salama. Ukiona mtoto wa mtu yupo katika mazingira ambayo yanakupa mashaka usiache kuhoji ili kujua usalama wake maana watoto hawa ndio tegemezi kwa jamii na nchi yetu”. Alieleza kijana huyo kwa hisia sana.
Mmoja kati ya vijana waendesha Bodaboda